
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametoa pole kwa familia,Jeshi, Bunge na Wananchi wa Jimbo la Ushetu kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Mhe. Elias John Kwandikwa.
Nasikitika kuwajulisha kuwa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias Kwandikwa amefariki dunia. Nitakumbuka umahiri wake katika uongozi na uzalendo. Natoa pole kwa familia, Jeshi, Bunge na wananchi wa Jimbo la Ushetu.
“Tumempoteza mtu muhimu ambaye mchango wake katika utumishi wa umma hautasahaulika. [Elias] Kwandikwa alikuwa kiongozi shupavu ambaye alikuwa akitekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria na taratibu. Mungu amweke mahali pema peponi, Amina.” amesema Rais Samia Suluhu Hassan.
