
Mamlakaa ya ajira imemsimamisha kazi muuguzi Scholastica Leoni Khanje wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mount Meru Arusha kwa kitendo cha kufanya mzaha katika zoezi la utoaji chanjo ya UVIKO-19 nchini.
Muuguzi Scholastica Khaje alionekana akiigiza kumchoma sindano Bwa.Abdallah Hemed Kwesiga ambaye ni Mkuu wa Idara ya Elimu ya Msingi wa Halmashauri ya jiji la Arusha na kusambaza katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Catherine Sungura imeeleza kusikitishwa na kitendo hicho na kuelekeza Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania kuchukua hatua Stahiki.
