×

Mkuu wa Wilaya Hanang Apokea Madawati ya Sekondari ya Katesh

Mkuu wa Wilaya ya Hanang Janeth Mayanja leo amepokea meza 50 na viti 50 kwa ajili ya sekondari ya Katesh, kutoka kampuni ya Bonanza Co.Ltd inayojihusisha na mchezo wa kubahatisha ikiwa ni harakati za kuhakikisha watoto wote wanakaa sehemu salama.

 

Mkuu wa Wilaya amewashukuru na kuwapongeza kwa kurudisha sehemu ya faida ambalo ni takwa la kisheria (yaani Corporate Social Responsibility) kwa jamii katika Wilaya Hanang.

Pia Mkuu wa Wilaya amewakumbusha kuwa biashara ya michezo ya kubahatisha nchini inaonekana kama biashara yenye mtazamo hasi lakini biashara hiyo ni biashara kama zilivyo biashara zingine ifahamike kwa kurudisha sehemu ya faida itaifanya jamii kuchukulia biashara hiyo kwa mtazamo chanya.

Kampuni ya Bonanza Co.Ltd wamehimizwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni na wamekumbushwa hairuhusiwi vijana wenye umri chini ya miaka 18 kushiriki katika michezo hiyo na Mkuu wa Wilaya amewaeleza Bonanza Co.Ltd atachukua hatua za kufunga biashara hiyo ya michezo ya kubahatisha ikiwa taratibu hazitafuatwa katika Wilaya ya Hanang.

Kwa upande wake Bw Haji Zonal Meneja wa kampuni ya Bonanza Co.Ltd ameahidi kufuata sheria na kuendelea kuchangia huduma za elimu na afya katika kurudisha faida kwa jamii.

Leave a Comment