×

Katibu Mkuu CCM Atoa Siku 14 Kwa Viongozi Ngazi Ya Mikoa ,Wilaya

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo ameagiza ndani ya siku 14 vingozi wote wa Chama hicho na kamati zao za siasa kuanzia Mkoa na Wilaya kushuka chini kukagua miradi yote ya maendeleo inayowazunguka.


Chongolo ametoa maagizo hayo leo Agosti 10,2021 mkoani Morogoro wakati akikagua mradi wa ujenzi wa reri ya kisisasa SGR.


“Niwapongeze watu wa Morogoro kwani mmeweza kuonyesha njia nami nimeamka Nije hapa na secretarieti yangu kujionea je kinachofanyika hapa ni kile kinachoubiliwa,”amesema Chongolo na kuongeza “Haya ni maagizo na maelekezo Kama tulivyopeana mara baada ya mkutano mkuu maalum kuwa wote tushuke chini kukagua miradi ya Maendeleo katika Maeneo yetu .”


Amesema wao wanawajibu wa  kuisimamia Serikali na utekelezaji wa Ilani kwani sisi ndio tutakaorudi kuwaeleza wananchi nini tumefanya

 


Kwa upande wake Mkurungezi Mkuu wa Shirika la Reli nchini (TRC) Masanja Kadogosa amesema anaishikuru Serikali kwa kuwapatia fedha kwa wakati kwa ajili ya kukamilisha mradi huo huku akifafanua mpaka sasa wamelipa  hati 34 kati ya 35 huku hiyo moja ambayo inalipwa muda wowote kuanzia sasa.


Wakati huo huo  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Martin Shegela  amesema uongozi wa mkoa huo umeridhishwa na kasi ya ujenzi kwani waliweza kutembelea eneo la kuanzia Kilosa mpaka Morogoro Station.


Amesema kuwa mradi huo umekuwa kichocheo kikubwa Cha uchumi wa Morogoro kwani wamekuwa wakitumia malighafi na bidhaa nyingi kutoka mkoa huo.

 

Leave a Comment