
Rais Samia Suluhu Hassan amesema alitaka kukutana na viongozi wa vyama vya siasa, lakini si wakiwa wamechambuka chambuka, kwa sababu wana vyama vyao vidogo vidogo na mabaraza yao, hivyo alitaka kwanza wajiunde kwenye baraza lao ambalo lilifanya uchaguzi wiki chache zilizopita kisha apange namna kukutana nao na kujadili kuhusu mwelekeo wake na ushirikiano katika kuijenga nchi.
Rais Samia alieleza hayo kwa mara kwanza katika mahojiano na Shirika la Utangaza la Uingereza (BBC), yaliyoongozwa na mtangazaji mwandamizi wa kituo hicho, Salim Kikeke kutoka Ikulu, Dar es Salaam na kurushwa jana Jumatatu, Agosti 9, 2021.
“Tumemaliza uchaguzi serikali imeundwa tunahitaji kuungana pamoja na kujenga nchi, lakini kinapotokea chama chao wanataka kuitisha maandamano tu, leo mkutano huku kesho kule, fujo, vurugu kila siku, kupiga magari, choma mali hapana kwa kweli.”
Alisema kwa vile wameshafanya uchaguzi na kamati zao ndogo zimejiunda vizuri, atatafuta siku ya kuzungumza nao. Alisema hata yeye anataka kuzungumza nao ili kuwaeleza mwelekeo wake baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa 2020 kwa kuwa katika harakati za kujenga nchi hachagui; akimuona mpinzani ana mwelekeo mzuri atamweka katika Serikali ili kujenga Taifa.
Alibainisha kuwa hakuna sehemu yoyote inayoeleza kuwa baada ya uchaguzi, chama kilichoshinda ndicho kitakachojenga nchi peke yake. “Mtanzania yeyote mwenye mtazamo mzuri wa kisiasa, anayeweza kutimiza majukumu yake na kuleta yale wananchi wanayoyahitaji, namtumia tu. Namwingiza kwenye mfumo wangu, twende.
“Nataka waje tukae tuone tunakwendaje na hili, na hii ni kwa sababu hakuna sehemu yoyote ile ilipoandikwa kuwa chama kilichoshinda pekee ndio kitajenga nchi, ni Watanzania wote ndio wataojenga nchi… ” alisema Rais Samia.
Kuhusu Uhuru wa Vyombo vya Habari
“Wewe Mwandishi wa Habari toka umefika umesikia Vyombo vya Habari vinalalamika? Hakuana chombo kinalalamika kuna uhuru wakutosha wakujieleza na wanajieleza Mpaka wanavuka Mipaka saa zingine….
“Wakati mwingine kusema kwao, bora umpe mtu nafasi aongee alichonacho, atoe umsikie. Kama kiongozi useme kinalalamikiwa hiki, basi unakifanyia kazi kuliko ukiwabana. Hujui wanafukuta na nini ndani. Tanzania kuna uhuru wa kutosha vyombo vyote vya habari…” alisema Rais Samia.
View this post on Instagram