×

Mbowe Alikimbia Nchi, Tuiachie Mahakama Iuonyeshe Ulimwengu – Video

Wakati Rais Samia Suluhu Hassan akisema, uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ulianza Septemba mwaka jana, lakini ulikuwa haujakamilika, amefafanua kuwa mashtaka yake hayakuchochewa kwa sababu za kisiasa.

 

Mkuu huyo wa nchi alisema anachojua ni kuwa Mbowe alifunguliwa kesi Septemba mwaka jana, akiwa na wengine kwa mashtaka ya ugaidi na uhujumu uchumi. Hata hivyo, alisema kwa wenzake kesi zao zilishaanza kusikilizwa, lakini Mbowe upelelezi wake ulikuwa haujaisha.

Rais Samia alieleza hayo kwa mara kwanza katika mahojiano na Shirika la Utangaza la Uingereza (BBC), yaliyoongozwa na mtangazaji mwandamizi wa kituo hicho, Salim Kikeke kutoka Ikulu, Dar es Salaam.

 

“Tumeingia kwenye uchaguzi, tumemaliza. Sasa polisi wamemaliza uchunguzi wao wamemhitaji kwa ajili ya kuendelea na kazi yao. Lakini kama utakumbuka Mbowe hakuwa nchini kwa kipindi kirefu, alikuwa amekimbilia Nairobi, aliporudi nchini kaitisha maandamano/ madai ya katiba nadhani alikuwa anajua ana kesi.

 

“Hii vurugu aliyokuwa anafanya nadhani yalikuwa na mahesabu akijua kuwa ana kesi ya namna hiyo na hii vurugu anayoianzisha, alitaka akikamatwa asingizie kuwa ni kwa sababu anadai Katiba mpya, sina uhakika lakini.

 

Samia alisema suala la Mbowe lipo mahakamani hana uhuru wa kulizungumzia kwa kina, huku akishauri jambo hilo liachwe katika chombo hicho cha kutenda haki ili kifanye kazi yake na kuuonyesha ulimwengu kama shutuma za Mbowe za kweli au la.

 

“Kwa sababu jambo liko mahakamani (tuhuma za ugaidi dhidi ya M/kiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe) sina uhuru wa kulizungumzia kwa sana. Nadhani tuache mahakama zioneshe ulimwengu kwamba hizo shutuma walizomshutumu ni za kweli au si za kweli…”amesema Rais Samia Suluhu.
 

 

Agosti 6 mwaka huu, Mbowe ambaye ni kiongozi wa zamani wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB) na wenzake watatu walisomewa mashtaka sita yakiwemo ya kufadhili vitendo vya ugaidi na kukusanya pesa kwa kufanya vitendo hivyo.

 

Mashtaka mengine ni kukusanya fedha kwa ajili ya kufanya vitendo vya kigaidi, kukutwa na silaha aina ya bastola na kukutwa na sare za jeshi kinyume cha sheria. Kati ya mashtaka hayo sita, Mbowe anakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kula njama na kufadhili vitendo vya kigaidi.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

Leave a Comment