×

Gazeti la Uhuru Lasimamishwa, Watatu Wasimamishwa Kazi – Video

KATIBU Mkuu wa Chama Cha mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ametangaza kusitishwa kwa uchapaji wa gazeti linalomilikiwa na chama hicho, gazeti la Uhuru kwa muda wa siku 7 kufuatia upotoshaji wa maneno yaliyodaiwa kusemwa na Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa mahojiano yake na Kituo cha BBC na kuchapishwa katika gazeti hilo, toleo la leo Agosti 11, 2021.

 

Akizungumza na wanahabari jijini katika Ofisi ndogo za CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, Chongolo amesema Bodi ya Uhuru Media Group yawasimamisha kazi Ernest Sungura -Mkurugenzi Mtengaji, Athumani Mbutuka -Mhariri Mtendaji, Rashid Zahoro -Msimamizi wa Gazeti la leo kufuatia kwa madai kuwa wamehusika moja kwa moja na upotoshaji huo.

 

Katika habari yake kuu limeandika kichwa cha habari “Sina wazo kuwania urais 2025- Samia” Huu ni upotoshwaji mkubwa na kumlisha maneno Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan. Aidha, kwa niaba ya CCM, Chongolo amemuomba radhi Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na chapisho hilo.

Kuhusu Uhuru na Demokrasia

“Mambo yanayodaiwa kwenye katiba mpya na wanasiasa ni machache sana, kwanza ni Tume Huru, pili ni uhuru wa kisiasa na demokrasia, hivi Tanzania haina uhuru? Ukitembelea nchi ambazo hazina uhuru utajua Tanzania tuna uhuru wa demokrasia.

 

“Wapi uliona wananchi wamedai katiba mpya, dai la katiba mpya ni letu sisi wanasiasa, hivi kupitia kupatikana kwa katiba mpya itawaletea wananchi unga? Katiba mpya inayodaiwa na wanasiasa ni kwa ajili ya kutengeneza nafasi za uongozi na madaraka.

 

Kuhusu Elimu

“Tumekuwa tukisubiria hadi mwezi Desemba ndio tunaanza maandalizi ya kuandaa miundombinu ya kujifuzia, sasa tumeielekeza serikali itenge fedha hizo kwenye robo ya kwanza ya mwaka wa fedha nasi tusimamie utekelezaji.

 

“Tangu tulipoteuliwa tulikuwa na kazi ya kutembea nchi nzima, na tulifanya kazi mbili, moja ni kujenga chama na pili ni kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kazi hiyo inaendelea.

 

“Suala la miundombinu ya kujifunzia ikiwemo madarasa, madawati fedha zake zitatolewa katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha, lengo ni kuondoa usumbufu wa kukimbizana na watendaji hata kufikia hatua ya kuzuia likizo zao. Changamoto hii tunataka kuimaliza mapema.

 

“Ili zoezi la elimu bila malipo liwe na tija zaidi ni lazima kuwe na miundombinu rafiki kwa wanafunzi, kwamba wanafunzi wanapoandikishwa waikute miundombinu yote ya kujifunzia inakuwa tayari,” amesema Chongolo.

 

Leave a Comment