
MUIGIZAJI wa kitambo ambaye aliwahi kujikita katika uandaaji wa matamasha ya muziki wa Injili, Muna Love, ametangaza kufanya upasuaji katika mwili wake ili kujiongezea mvuto wa kimuonekano.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Muna ameweka kipande cha video kinachomuonesha akifanyiwa upasuaji huo usoni kutengeneza ‘dimpoz’ na kusindikiza na ujumbe huu.

‘‘Nilikua napenda dimpoz msema kweli mpenzi wa Mungu staki maswali. Hii ilikua surgery ya pili katika nne nilizofanya tiari, Ntawaletea ya tatu nimefanya nini.
Saiv tukikutana ninatabasamu ata mkiniuzi ili muone dimpoz ya uso sasa ndo mtafurahi. God is Good to me. I love you Jesus.’’
Kwenye posti yake nyingine, Muna ameweka picha yake mpya ikimuonesha akiwa na dimpoz na kudai kuwa amefanya upasuaji huo wa tatu na amepanga kufanya upasuaji katika maeneo tofauti mara 11.

Muna aliwahi kuwa shoga mkubwa wa muigizaji Wema Sepetu kisha baadaye walitibuana. Kwa sasa, Muna amekuwa akiposti vipande vya video akicheza muziki wa Injili lakini hata hivyo amekuwa akikosolewa kutokana na mavazi yake tata huku akidai ameokoka.
Written by
@erick.evarist cc
@hotpot_tz