×

Waziri Aweso Ateua Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amemteua CPA Joyce Msiru kuwa Mkurugenzi wa mamlaka za maji nchini. Bi. Joyce Msiru alikuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) mkoani Mara. Uteuzi huo umefanyika leo wakati akizindua miradi ya maji Mji mdogo Shirati baada ya kufurahishwa na utendaji kazi wake.

 

Leave a Comment