×

Ligi Kuu England Moto Kuwaka Leo na Kesho

PAMOJA na Ligi Kuu England kutarajiwa kuendelea leo kwa michezo kadhaa, mashabiki wanasubiri kwa hamu mchezo mkali wa kesho.


Kesho mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England, Man City wanatarajiwa kujitupa uwanjani kupambana na Tottenham
Hotspur.

City walichukua ubingwa wa ligi hiyo msimu uliopita, lakini Spurs ilikuwa timu ambayo ilitoa upinzani mkali zaidi baada ya kumaliza ligi ikiwa kwenye nafasi ya
saba.


Arsenal walifungua msimu usiku wa kuamkia leo walipovaana na Brentford wakiwa ugenini.Michezo mikubwa ya leo, Man United watavaana na Leeds kwenye mchezo wa
mapema sana.


Huu unatajwa kuwa mchezo mkali sana kutokana na ubora wa Leeds msimu uliopita lakini pia kiwango cha mastaa
ambao wamesajiliwa Man United.


Mechi nyingine kali itakuwa ni ile ya Chelsea na Crystal Palace, pamoja na Liverpool dhidi ya Norwich.
Spurs hawajafanya usajili mkubwa sana lakini wanatajwa kuwa wanaweza kuwapa upinzani mkali Man City ambao
wamesajili mastaa kadhaa akiwemo Jack Crealish na wanaweza kukamilisha usajili wa Harry Kane muda wowote kuanzia sasa.

Leave a Comment