×

Huyu Ndiye Bruno Fernandez

WAKATI mashabiki wa Arsenal wakiwa hawana furaha kabisa kwa mwendelezo wa kufanya vibaya, wale wa Man United wenyewe wana tabasamu kwa kile alichokifanya Bruno Miguel Borges Fernandes; mtu na nusu kutoka Kusini Magharibi mwa Bara la Ulaya huko Ureno.

 

Alifunga hat-trick (mabao matatu) kwenye ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Leeds United katika ufunguzi wa Ligi Kuu England.

 

Mabao mengine yaliwekwa kambani na Greenwood na Fred; shukrani ziende kwa Paul Pogba aliyetoa msaada (assists) za mabao manne.

 

Uwezo Bruno Fernandez kwenye mpira wa miguu unaturudisha nyuma yapata miaka kumi na mitano iliyopoita hadi 2006 ambapo binadamu wa kuitwa Cristiano Ronaldo alifanya maajabu pale OT (Old Traford).

 

Mwaka 2013 Bruno Fernandes aliaga soka la nyumbani klabuni Novara na akapanda merikebu ya kusaka neema kunako Seria A pale Udenese kisha Sampdoria.

 

Safari yake ilisongwa na misukosuko kanakwamba hakuaga wazee na mababu zake. Safari yake ilikuwa ngumu akibugikwa na jasho la kukaa benchi.

 

Alipata ufinyu wa kucheza kiasi cha kusababisha kuona kuwa mcheza kwao hutuzwa Euro milioni 8.5 zilitosha kumruhusu kushuka Merikebu ya Sampdoria na kuvuka Kunako Meli ya Sporting CP Lisbon.

Kuta na Minara ya Lisbon zilimbadilisha rangi na kuwa Bruno  meli yake ya Seria A na Lisbon ilifikisha mabao 83 na assist 70 akiwa amecheza mechi 291.

Bruno Fernandez anatajwa na mashabiki wa United kama Ronaldo mwingine pale OT akitokea Sporting CP.

Sifael Paul

Leave a Comment