
Rais Samia Suluhu Hassan amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu, Lilongwe nchini Malawi kushiriki Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajiwa kuanza hapo kesho Agosti 17 hadi Agosti 18 nchini Malawi.
Pamoja na mambo mengine, mkutano huo pia utaithibitisha Malawi kuwa Mwenyekiti wa SADC kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Agosti 2021 hadi Agosti 2022.