
WAZIRI wa Madini, Doto Biteko ameiagiza Kampuni ya kuzalisha Gesi Asilia ya Kabon Daioksaidi ya Tol Gases Limited iliyopo wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya kufuata Kanuni na Taratibu zilizowekwa na Wizara ya Madini ikiwemo Kanuni ya Uchangiaji Maendeleo kwa Jamii (Local Content), Menejimenti ya Kampuni ya Uchimbaji Madini kuwepo eneo la mgodi pamoja na kutunza taarifa za mauzo ya madini.

Waziri Biteko amesema kuwa, marufuku kusafirisha gesi kutoka Kiwandani hapo bila kuwepo Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mbeya, Afisa wa Takukuru, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, pamoja na Afisa kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa wilaya ya Rungwe ili wafunge lakiri (Seal) kwa lengo la kudhibiti udanganyifu.

Akizungumza baada ya kufanya ziara katika Kiwanda hicho, Waziri Biteko amesema kuna baadhi ya taarifa za mauzo zinazoonesha kiasi cha fedha kilichouzwa gesi hiyo hazipo kwenye kumbukumbu ya vitabu vya Kapuni hiyo ambapo ni kinyume na taratibu zilizowekwa na Wizara ya Madini.

Aidha, Waziri Biteko ameitaka Kampuni hiyo kuhakikisha Menejimenti ya Kampuni hiyo inakuwepo eneo la uzalishaji baada ya kugundua uongozi wote wa ngazi za juu upo jijini Dar es Salaam ambapo Sheria ya Madini inasema sehemu yoyote inayochimbwa madini menejimenti iwepo na takwimu zote ziwepo mgodini.

Pia, Waziri Biteko ameitaka Kampuni ya Tol Gases Limited kuhakikisha inachangia maendeleo kwa jamii katika eneo linalozunguka mgojamii ione manufaa ya Gesi iliopo katika mazingira yao.


