×

Mama Aanika Alipo Baba wa Romy Jons

JUMAMOSI iliyopita, Agosti 14, 2021 ilikuwa Birthday ya Dj maarufu Bongo, namzungumzia @romyjons ambaye pia ni kaka wa Staa wa Bongo Fleva, @diamondplatnumz.

 

Swali lililokuwa zito kwa Mama mzazi wa Romy wakati wa hafla hiyo ilikuwa ni kuwaeleza mashabikiwa mwanae pamoja na Watanzania wote kwamba ni wapi alipo baba mzazi wa Romy ambaye hajawahi kutajwa wala kuonekana kama.

 

Mama Romy amejibu na kusema; “Nilimzaa Romy kabla ya kuoana na baba yake, baadaye tulikuja kuoana wakati Romy akiwa na umri wa miaka miwili. Baadae mume wangu alisafiri kwenda nchini Italy ambapo bahati mbaya alipatwa na matatizo.

 

“Mawasiliano yalikuwepo baina yetu lakini baada ya siku kama mbili tangu kuwasiliana kwetu nilipata taarifa kuwa mume wangu  amedondoka chooni na kufariki dunia.

 

“Mwili ulirudi baada ya siku 28, hivyo ilinibidi kurudi nyumbani kwetu kumlea Romy kwani alikuwa mdogo bado, hapo nilianza kuhangaika kwenye mihangaiko yangu kumsomesha mwanangu na mara nyingi nilimuacha kwa mama mzazi wa Diamond kila nilipokuwa nikienda kwenye mizunguko yangu ya biashara,” alisema Mama Romy.

 

Leave a Comment