×

Rais Biden Agoma Kubeba Msalaba wa Afghan

Rais wa Marekani, Joe Biden ametetea uamuzi wake wa kuondoa majeshi yake nchini Afghanistan licha ya nchi hiyo kutekwa na Taliban.

 

Hata hivyo, Biden amekubali kuwa matokeo yaliyochangia Taliban kupindua serikali ya Afghan na kuchukua madaraka yalitendeka kwa “haraka sana kuliko ilivyotarajiwa”.

 

“Wamarekani hawawezi na hawastahili kupigana vita au kufariki dunia katika vita ambavyo Waafghan wenyewe hawako tayari kujipigania. Nitaendelea kusimamia uamuzi wangu,” Biden amesema kutoka Ikulu ya Marekani.

 

Jumapili, Agosti 15, Taliban walitangaza ushindi baada ya Rais wa Afghan, Ashraf Ghani kutoroka nchi na serikali huku wanamgambo wa Taliban wakiingia Ikulu.

 

Wanamgambo wenye msimamo mkali wanarejea serikalini baada ya karibu miaka 20 ya uwepo wa Muuungano ulioongozwa na Marekani ambao umeshindwa.

Biden anakabiliwa na ukosoaji mkubwa wa kisiasa kutokana na uamuzi wake wa Aprili kuagiza wanajeshi wote wa Marekani kuondoka Afghanistan kufikia Septemba 11, maadhimisho ya miaka 20 tangu kutokea kwa shambulizi lililochochea Marekani kuvamia nchi hiyo.

Leave a Comment