
WAKATI kikosi cha Simba kikiendelea na mazoezi ya kujiandaa na michuano mbalimbali kwa msimu ujao ikiwemo Ligi ya Mabingwa Afrika, timu hiyo inatarajia kucheza michezo ya kirafiki dhidi ya timu za Morocco.
Simba waliondoka nchini Agosti 10, mwaka huu kwenda Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya uliopangwa kuanza mwishoni mwa Septemba mwaka huu na wamepanga kuwa huko kwa wiki mbili.
Inasemekana kuwa Simba ikiwa Morocco itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya FAR Rabat ya nchini humo ambayo inanolewa na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroek.

Sven ambaye aliipa Simba ubingwa wa Kombe la Ligi Kuu na la Shirikisho la Azam (ASFC), kwa msimu wa 2019/20 huku pia akichangia katika kuipa Simba Kombe la ligi kwa msimu wa 2020/21.
Akizungumza na Championi Jumatano, kutokea nchini Morocco, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu alisema kuwa timu inaendelea vizuri na mazoezi.“Tunamshukuru Mungu tupo salama na tunaendelea vizuri na maandalizi kabla ya msimu ujao.
Ni kweli tutakuwa na mechi za kirafiki ila kujua ni nani tutacheza naye na lini ila bado tunapanga.“Idadi itategemeana na ratiba pamoja na upatikanaji wa hizo mechi tukiwa huku na tutacheza na timu za huku Morocco ili kujipima nguvu,” alisema Rweyemamu