×

Dk Gwajima: Eti Mimi Kigeugeu, Ninabadilika Badilika? Hili Agano Jipya

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Doroth Gwajima amesema hakuna kilichobadilika kutoka awamu ya tano kuja awamu ya sita ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kupambana na janga la corona.

 

Dk. Gwajima amesema hayo leo Alhamisi, Agosti 19, 2021 wakati akizungumza na watumishi wa afya mkoani Geita na kuongeza kuwa Hayati Dkt. John Magufuli alianzisha harakati za kupambana na janga hilo na Rais Samia Suluhu amekuja kuendeleza alichokianzisha Magufuli.

 

“Eti mimi ni kigeugeu, ninabadilika badilika, mimi sijabadilika, tulitekeleza mambo ya tiba asili tuliyoambiwa kwenye awamu ya tano, (chini ya Hayati Magufuli) na kwamba tusipokee chanjo bila kujiridhisha, tumekuja awamu ya sita tunatekeleza tuliyopewa awamu ya tano.

 

“Agano la kale la awamu ya tano na agano jipya la serikali ya awamu ya sita sio kwamba agano jipya limekuja kufuta agano la kale. Ukiona mtu anasema nabadilika badilika mwambie tu wewe huelewi kama wale wa darasani ambao huwa hawaelewi, asubiri NECTA ikirudiwa labda ataelewa kwa sababu alikuwa analala darasani.

 

“hao wanaopiga kelele tayari wameshakwenda Ulaya wakachanja, sasa muwaulize walifikaje Ulaya, za kuambiwa ongeza na za kwako,” amesema Dk. Gwajima.

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

Leave a Comment