×

Varane: Tutasaidiana na Pogba Kutwaa Makombe

BEKI mpya wa Manchester United, Raphael Varane amesema yeye na kiungo Paul Pogba watahakikisha wanaipa mafanikio timu hiyo.


Varane alianza mazoezi na timu
hiyo juzi akiwa amesajiliwa kwa kitita cha pauni milioni 42, akitokea Real Madrid ya nchini Hispania.


Beki huyo ameonekana kufurahia
kujiunga na timu hiyo na kumkuta Pogba ambaye wanacheza pamoja kwenye timu ya Taifa ya Ufaransa. Akizungumza kwa mara ya kwanza klabuni hapo, Varane amesema yeye pamoja na Pogba watahakikisha kuwa timu hiyo inatwaa makombe makubwa.

 

“Kumekuwa na tetesi nyingi sana kuhusu mimi na Manchester United kuanzia mwaka 2011, kipindi ambacho kocha Alex Ferguson alikuja kwenye nyumba ya mama yangu.

 

Ni kweli kuwa tulizungumza na klabu yangu na nafikiri ulikuwa muda sahihi wa kucheza Ligi Kuu England kwangu kwa kipindi kile lakini ikashindikana.“Ninafuraha sana kuwa hapa kwa sasa nafikiri mimi na Pogba na wachezaji wengine hapa tutaisaidia timu hii kutwaa makombe makubwa,” alisema Varane.

AJALI MBAYA: WATU 10 WAFARIKI Baada ya GARI la JESHI KUGONGANA na FUSO la MIZIGO

Leave a Comment