×

Chadema Wasusa Kwenda Ikulu

 

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema haitashiriki hafla ya kukabidhi taarifa ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 itakayofanyika kesho Jumamosi, Agosti 21, 2021, Ikulu jijini Dar es Salaam na badala yake itaendelea kuweka nguvu zaidi katika ajenda zake za  kipaumbele.

 

Taarifa ya Chadema iliyotolewa leo Agosti 20, 2021 na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na mambo ya nje, John Mrema imesema wamepokea mwaliko kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), lakini hawatakwenda huku wakitoa sababu tano.

 

“Tumepokea mwaliko kutoka kwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya Mwenyekiti wa Taifa, Katibu Mkuu, Mgombea Urais na mgombea umakamu wa Rais kuhudhuria shughuli hafla ya kukabidhi kwa Rais taarifa ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020,” imesema taarifa hiyo.

Leave a Comment