×

Taliban Wapiga Msako Nyumba kwa Nyumba

Umoja wa mataifa umeeleza kuwa Taliban wako kwenye msako wa nyumba kwa nyumba kuwatafuta watu waliofanya kazi na vikosi vya Nato au serikali ya zamani ya Afghanistan.

 

Kundi hilo lenye msimamo mkali wa kiislamu tangu kutwaa madaraka limeahidi kuwahakikishia Waafghan kuwa hakutakuwa na kisasi lakini kuna hofu kwamba Taliban wamebadilika kidogo tangu miaka ya ukatili ya 1990.

 

Katika mkutano wao wa kwanza na waandishi wa habari kikundi hicho kimeahidi kuwa haki za wanawake zitaheshimiwa.

Leave a Comment