
MWILI wa aliyekuwa mchambuzi nguli wa soka Tanzania, Mwalimu Alex Kashasha (64) leo Jumatatu, Agosti 23, 2021, umepumzishwa kwenye nyumba yake ya milele katika Makaburi ya Kinondoni.

Mwalimu Kashasha alifariki dunia Alhamisi, Agosti 19, 2021 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam. Kashasha alikuwa mtumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) hadi umauti ulipomfika.