Rais Samia Awasili Zambia Kuhudhuria Sherehe ya Kuapishwa Rais Mpya
Global Publishers August 24, 2021 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Zambia alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Keneth Kaunda Jijini Lusaka Zambia leo Agosti 24, 2021 kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe ya kuapishwa Rais Mpya wa 7 wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Agosti 24, 2021 amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa, Keneth Kaunda, jijini Lusaka Zambia kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe ya kuapishwa Rais Mpya wa 7 wa nchi hiyo, Hakainde Hichilema.