MTU mmoja aliyejihami kwa bunduki ameuawa baada ya kuwaua askari wawili katika majibizano ya risasi mkoani Dar es salaam. Kwa mujibu wa Mkuu wa Polisi nchini Simon Sirro, tukio hilo limetokea katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi.
Awali Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ulitoa tahadhari ya dharura kufuatia kudhibitiwa kwa mtu huyo katika maeneo ya daraja la Salenda nje ya ubalozi wa Ufaransa.

Mtu huyo aliyekuwa amejihami na bunduki aina ya AK 47 alikuwa amesimamia nje ya ubalozi huo huku akionekana kuyaelekeza magari yaliokuwa yakipitia barabara hiyo.
Hatahivyo polisi waliarifiwa na kumkabili jamaa huyo ambaye aliwaua maafisa wawili wa polisi. Ubalozi huo umetoa wito kwa raia wake kuchukua tahadhari na kutotumia barabara ya tukio hilo.
Hatahivyo polisi waliarifiwa na kumkabili jamaa huyo ambaye aliwaua maafisa wawili wa polisi. Ubalozi huo umetoa wito kwa raia wake kuchukua tahadhari na kutotumia barabara ya tukio hilo.