
RAIS Samia Suluhu Hassan, ametoa pole kwa familia za askari watatu na askari mmoja wa Kampuni ya Ulinzi ya SGA waliopoteza maisha baada ya mtu aliyekuwa na silaha kuwashambulia katika eneo la Salenda jijini Dar es Salaam.
Rais Samia amesema mtu huyo amedhibitiwa na hali ni shwari na kuwaagiza polisi kuchunguza kwa kina.
Salamu hizo za pole za Rais Samia, zinakuja kufuatia tukio la mtu aliyekuwa na silaha ambaye naye ameuawa na polisi, kuwashambulia kwa risasi na kuwaua askari waliokuwa katika Makutano ya Barabara za Kenyatta na Ali Hassan Mwinyi, jirani na Ubalozi wa Ufaransa, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Watu sita wamejeruhiwa na wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
