×

Kesi ya Mbowe, Mahakama Yakataa Mapingamizi ya Serikali – Video

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo Agosti 30, imeanza kusikiliza Kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe dhidi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
 
Mahakama Kuu kanda ya DSM chini ya Jaji John Mgetta imetupilia mbali mapingamizi manne yaliyowasilishwa na Jamhuri katika kesi Na. 21/2021 iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe. 

Miongoni mwa mapingamizi ni kutaka kesi hiyo iondolewe Mahakamani kwa kuwa utaratibu uliotumika kufungua kesi hiyo umekiuka sheria huku wakiomba mapingamizi hayo yasikilizwe kwa maandishi mbele ya Jaji John Mgeta.

 

Mapingamizi hayo yamewasilishwa na Wakili Mkuu wa Serikali Hangi Chang’e huku upande wa Mbowe ukiwakilishwa na Jopo la Mawakili Saba wakiongozwa na Peter Kibatala ambao wamesema hawana pingamizi na hoja za Serikali.

 

Baada ya kutoa hoja hiyo, Jaji Mgeta akatoa utaratibu wa namna pande zote mbili kuwasilisha hoja zao ambapo Pande zote zinatakiwa kuwasilisha hoja Septemba 6, 9 na 13, 2021 kwa njia ya maandishi na hukumu kutolewa Septemba 23, 2021.

 

Aidha, Kesi ya Mbowe anayokabiliwa na mashtaka ya ugaidi inatarajiwa kuendelea kesho Jumanne, Agosti 31, 2021 katika Mahakama Kuu – Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu (maarufu kama Mahakama ya Mafisadi) iliyopo katika Chuo cha Sheria, Ubungo Mawasiliano jijini Dar es Salaam.

Leave a Comment