
KIMBUNGA kikali, Ida kimesababisha madhara makubwa nchini Marekani ikiwa ni pamoja na kuvunja majengo na kuvuruga huduma ya nishati kwenye jimbo la Louisiana.
Rais Joe Biden ameahidi msaada kwa waliokumbwa na maafa amesema serikali itaendelea kutoa msaada kwa kadri itakavyohitajika.
Watabiri wa hali ya hewa wamekiainisha kimbunga Ida kuwa cha hatari kubwa kutokana na upepo wake kuwa na kasi ya zaidi ya kilometa 240 kwa saa.
Serikali ya Marekani imewataka watu wanaoishi kwenye maeneo ya pwani waondoke na kutafuta hifadhi kwenye maeneo salama.
Dhoruba hiyo pia imesababisha mafuriko, kwa mujibu wa taarifa ya gavana wa jimbo la New Orleans John Bel Edwards mpaka sasa mtu mmoja amekufa baada ya nyumba yake kuangukiwa na mti.