
JESHI la Marekani kwa kutumia ndege zake zisizo na rubani katika Mji Mkuu Kabul limefanikiwa kuzima shambulio jingine baya la kujitoa muhanga katika uwanja wa ndege ikiwa ni siku chache tangu uwanja huo kushambuliwa na kuua watu 13 wakiwemo wanajeshi watatu wa marekani, maafisa wa jeshi la Marekani wamesema.
Shambulio hilo lililenga gari lililobeba mtu mmoja anayehusishwa na kundi la Islamic State, tawi la Afghanistan, jeshi la Marekani limeeleza. Marekani ilionya juu ya uwezekano wa mashambulio mengine wakati operesheni za kuondoa raia zikitamatika. Pamoja na hayo, imesema kuwa itaendelea kuwaondoa Waafghan kutoka uwanja wa ndege wa Kabul mwisho.
Tarehe ya mwisho ya ujumbe wa uokoaji ya Agosti 31 ilikubaliwa kati ya Marekani na Taliban, ambao sasa wanadhibiti sehemu kubwa ya nchi. Marekani itakuwa ya mwisho kumaliza kazi yake, na nchi nyingine zote tayari zimekamilisha zao. Ndege za mwisho zinazowarudisha wanajeshi wa Uingereza kutoka Afghanistan zimekuwa zikiwasili nchini Uingereza siku ya Jumapili.
Marekani inasema imewezesha uokoaji wa watu zaidi ya 110,000 kutoka uwanja wa ndege wa Kabul tangu tarehe 14 mwezi Agosti – siku moja kabla ya Taliban kuchukua udhibiti wa mji mkuu.

Maafisa wa ujasusi wa Marekani mapema walisema wamepokea vitisho ”, vya kuaminika” dhidi ya uwanja wa ndege, na kwamba wanajeshi wataendelea kutekeleza mashambulizi pale inapobidi. Marekani ilishauri watu kukaa mbali na eneo hilo, licha ya muda kuisha kwa mtu yeyote anayejaribu kupata ndege za uokoaji.
Kando na hayo, Jumapili, polisi wa Kabul walisema mtoto alikuwa ameuawa katika shambulio la roketi kwenye nyumba karibu na uwanja wa ndege. Maelezo kuhusu shambulio hilo hayajawekwa wazi. Shambulio la bomu katika uwanja wa ndege Alhamisi iliyopita liliua watu 170, pamoja na wanajeshi 13 wa Marekani.
Kundi la , IS-K, lilikiri kutekeleza shabulio la Alhamisi. Kwa kulipiza kisasi, Marekani ilifanya mashabulizi ya ndege zisizo na rubani mashariki mwa Afghanistan Ijumaa, ikisema imeua wafuasi wawili “wa juu” wa IS-K.

Rais wa Marekani Joe Biden Jumapili alikutana na familia za wafanyikazi 13 wa Marekani waliouawa katika shambulio la uwanja wa ndege wa Kabul Alhamisi. Biden alishiriki katika hafla ya heshima kwa waathiriwa katika kituo cha Jeshi la Anga la Dover huko Delaware.
Mbali na wanajeshi wa Marekani waliouawa katika shambulio la bomu la IS-K, makumi ya Waafghan ambao walikuwa wamepanga mstari kwenye uwanja wa ndege kwa matumaini ya kuondoka nchini humo pia walipoteza maisha.
Raia wawili wa Uingereza na mtoto wa raia wa Uingereza walikuwa miongoni mwa waliokufa. Wengi wa watu wenye itikadi kali wa IS-K wanaaminika wamejificha katika mkoa wa Nangarhar nchini Afghanistan, mashariki mwa Kabul.