×

Kifo Cha Msanii Chaacha Simanzi Rwanda

KIFO cha ghafla cha msanii nyota muziki wa Hip hop nchini  Rwanda, Joshua Tuyishime ‘Jay Polly’, aliyefariki ghafla akiwa hospitalini jijini Kigali kimeacha simanzi nzito miongoni mwa mashabiki wake.

 

Wakati watu wakiendelea kutafakari juu ya kile kilichopoteza maisha ya msanii huyo, vyombo vya habari nchini humo zilisema kuwa Joshua Tuyishime alikimbizwa hospitalini kutoka Gereza Kuu la Kigali baada ya kupatwa na ugonjwa usiojulikana Jumatano ya Septemba Mosi, 2021 usiku.

 

Jay Polly mwenye umri wa miaka 33 alikamatwa mwezi Aprili kwa makosa ya matumizi ya dawa za kulevya, na kesi yake ilikuwa inaendelea.

 

Kaka yake Maurice Uwera ameliambia Shirika la Habari la BBC kuwa mamlaka ya huduma za magereza nchini Rwanda, imemueleza kuhusu kifo chake, lakini hakutoa maelezo zaidi.

STORI NA RICHARD MANYOTA | GPL

Leave a Comment