×

Mbele ya Rais Samia, RC Makalla Afunguka – Video

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amekiri mafuriko ni tatizo kubwa kwa wakazi wa mkoa wake na kwamba serikali imeanza kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kufanya usanifu wa eneo la Namanga ambalo limekuwa kero hasa kila inaponyesha mvua.
“Usanifu umekamilika na ramani ni nazo, hapa namanga mafuriko yatabaki historia,” Makalla amemwambia Rais Samia Suluhu Hassan wakati akielekea Bagamoyo Mkoani Pwani. Makalla amesema eneo la Tegeta limepokea Sh bilioni 3.5 kuboresha soko na kwamba kuna bajeti kwa ajili ya kuboresha stendi ya mabasi ya abiria.

 

Leave a Comment