×

AzamFC Warejea Nchini

KIKOSI cha Azam FC kilichokwenda nchini Zambia kwa ajili ya maandalizi ya ligi msimu ujao kimerejea leo nchini.

Azam iliweka kambi ya siku 12 Zambia, katika Mji wa Ndola, ndani ya siku hizo walicheza michezo mitatu ya kirafiki.

Ambapo walianza na Red Arrows wakafugwa 0-4, wakacheza na Kambwe wakashinda bao 1-0, wakamalizia na Zesco na kuwafunga 1-0.

Akizungumza na Championi, Ofisa Habari wa Azam, Thabit Zakaria, amesema kuwa: “Tumamaliza maandalizi yetu na michezo ya kirafiki tuliyoipanga sasa ni muda wakurudi nyumbani tukazidi kujiandaa, tutaingia kesho (leo) Dar na kikosi kizima kilichoweka kambi Ndola,” alisema Zaka Zakazi.

CAREEN OSCAR, Dar es Salaam

 

Leave a Comment