
BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Idd Pialali amepoteza pambano la ubingwa wa UBO dhidi ya Arvi Avci kwa TKO raundi ya sita katika pambano lililopigwa Cafetaga Sports jijini Istanbul nchini Uturuki.
Katika pambano hilo ambalo lilikuwa la uzito wa Walter, Pialali amepoteza kwa TKO ya raundi ya sita katika pambano la raundi kumi.
Akizungumza na Champion jumatatu kocha wa Bondia huyo Edward Lyemike alisema :” Bondia wake alipoteza pambano hilo kwa sababu lilikuwa pambano la kushitukiza hakupata muda wakutosha kujiandaa kuelekea pambano hilo.
” Hata hivyo, ameomba radhi kwa Watanzania kwa kupoteza pambano na alisema mara baada ya kuwasili nchini tutaanza maandalizi ya pambano letu la mwezi Oktoba dhidi ya Bondia Ramadhani Shauri ambalo lazima tumkalishe, ombi langu kwa wapenzi na mashabiki wa masumbwi wazidi kuendelea kumuunga mkono kijana wao,” alisema Nicholaus.
JOSIAS JOSEPH (TUDARCO)