
TEKNOLOJIA ya kuhifadhi mayai ya uzazi ya mwanamke na manii ya mwanaume imeboreshwa na sasa utunzaji wa mayai hayo utaongezwa hadi miaka 55 chini ya mpango wa serikali ya Uingereza ambao mawaziri wanasema utawapa watu nafasi zaidi ya kuamua wakati wa kuanza familia zao.
Waziri wa Afya nchini humo, Sajid Javid amesema ukomo wa sasa wa miaka 10 ulikuwa na masharti makali. Teknolojia hiyo ya kisasa ya kugandisha inamaanisha kuwa mayai yanaweza kuhifadhiwa bila ukomo ili kuzuia mayai hayo kuharibika, utafiti wa Taasisi ya uzazi nchini Uingereza umedokeza.
Mpango huo unahitaji kuidhinishwa na bunge ambapo kwa sasa, miaka 10 ikiisha, wazazi wanatarajiwa lazima waamue ikiwa watafanyiwa tiba ya uzazi la sivyo seli hizo zitupwe.

Chini ya mfumo huo mpya, watapewa chaguo la kuweka au kutupa seli zilizohifadhiwa au kijusi kwa vipindi vya miaka 10. Javid amesema mabadiliko haya, yatachukuliwa na Serikali na ni hatua kubwa kuelekea sio tu kuwapa watu uhuru kuhusu uzazi wao, bali pia usawa.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya uzazi nchini Uingereza, Dkt Raj Mathur amemesema mpango huo ni thabiti na kwamba kurefushwa kwa ukomo wa muda kunalinda uwezo wa wahusika wote kufanya uamuzi wa uzazi wao wenyewe kama watu binafsi na wenza.
Kugandisha yai, manii na kijusi ni nini?
Ni njia ya kuhifadhi uzazi kwa kukusanya mayai, mbegu za kiume au kijusi na kuzihifadhi ili mzazi mtarajiwa aweze kupata mtoto siku za baadaye. Mchakato huo unahusisha kukusanya mayai 15 kupitia mfumo wa IVF, kuzipoesha na kisha kuzihifadhi katika tangi maalum lenye maji ya nitrojeni.

Mayai hayo halafu yatatumiwa wakati yanahitajika, lakni ni yale tu yatakayokuwa hai ndio yatatungishwa na manii. Sampuli ya manii kawaidi hugawanywa kati ya kontena kadhaa zinazofahamika kama mirija kabla ya kuzigandisha ili ziweze kutumika katika tiba tofauti.
Vijusi vinagandishwa wakati wa tiba ya uzazi ikiwa awamu ya kwanza haikufaulu unaweza kujaribu tena. Zinaweza kugandishwa kama seli moja, katika hatua ya seli mbili hadi nane au baadaye katika hatua ya ukuaji.