×

Coma Yamuua Adams wa PSG

MCHEZAJI wa zamani wa Ufaransa, Jean Pierre Adams ambaye alikuwa akiugua ugonjwa wa coma (kupoteza fahamu na kuongea) kwa miaka 39 amefariki akiwa na umri 73.

 

Adams alikuwa amelazwa hospitalini baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti lake mwezi Machi mwaka 1982 lakini hakupata tena ufahamu baada ya makosa ya daktari kukosea wakati wa kumdunga sindano ya usingizi kabla ya upasuaji.

 

Adams mzaliwa wa Senegal, alikuwa akicheza nafasi ya beki na alicheza zaidi ya mechi 140 akiitumikia Klabu ya Nicena pia aliichezea Klabu ya Paris St- Germain (PSG).

 

Katika Taarifa ya PSG imesema kwamba mchango wa mchezaji huyo unafaa kuheshimiwa huku Nice wakisema kwamba itaomboleza kifo cha Adams ambaye aliichezea Ufaransa mechi 22 kati ya mwaka 1972 -1976 kabla mechi iliotarajiwa dhidi ya Monaco Novemba 19.

 

Adams pia aliichezea Klabu ya Nimes 84, ambayo nayo imetuma salam za rambirambi kwa familia ya mchezaji huyo. Siku ambayo Adams alifanyiwa upasuaji baada ya kupata jereha la goti lake ambalo alipata wakati alipokuwa katika mazoezi ambapo wafanyakazi wengi wa hospitali katika klabu hiyo walikuwa katika mgomo.

 

Upasuaji wake ulifanyika huku daktari anayehusika na kudunga sindano ya ganzi (nusu kaputi) akihudumia wagonjwa wengine  wanane, ikiwemo Adams kwa wakati  mmoja.

 

Adams alisimamiwa na daktari aliyekuwa akijifunza, ambaye baadaye alisema kazi aliopatiwa alishindwa kuimudu jambo ambalo lilisababisha kosa kubwa na kumfanya Adams kupata mshtuko wa moyo na kuharibika ubongo.

 

Katikati ya mwaka 1990 ndipo daktari wa sindano za ganzi na mwanafunzi wake waliadhibiwa wakisimamishwa kazi kwa mwezi mmoja na kupigwa faini ya Euro 750.

 

Adams alitolewa katika hospitali hiyo baada ya miezi 15 na alikuwa akiangaliwa nyumbani Nimes na mkewe , Bernadettetangu wakati huo.

Leave a Comment