
MUIGIZAJI maarufu wa filamu kutoka nchini Marekani Michael Williams amefariki dunia. Nyota huyo amekutwa amefariki nyumbani kwake usiku wa Septemba 6, 2021.
Williams ni mmoja wa wasanii aliyekuwa mbioni kuwania nafasi ya kushiriki katika filamu ya maisha halisi ya marehemu DMX.
Polisi mjini New york wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha kifo cha msanii huyo.
Baada ya uchunguzi kufanyika kifo chake kinahusishwa na matumizi ya madawa ya madawa ya kulevya.