×

Mtoto wa Gaddafi Achiwa Huru


Mtoto wa tatu wa kiongozi wa zamani wa Libya, Muammar Gaddafi, ameachiwa huru kutoka jela ya mji mkuu wa Tripoli, ambako alikuwa amefungwa tangu mwaka 2014.

Sa’adi Gaddafi alikuwa kamanda wa kikosi maalum cha Libya lakini pia alikuwa maarufu katika uchezaji wa kandanda nchini Italia.

Alikimbilia Niger wakati baba yake alivyopinduliwa na kuuliwa mwaka 2011 lakini alirudishwa Libya ambako alikutwa hana hatia dhidi ya kesi zote zilizomkabili yakiwemo madai ya mauaji.

Muda mfupi baada ya kuachiwa huru bwana Gaddafi alikodisha ndege binafsi na kwenda Istanbul.

Serikali ya Libya imetoa taarifa kuwa walikuwa wana matumaini kuwa kuachiwa kwake kutaweza kusaidia taifa hilo kufikia katika makubaliano.

Leave a Comment