
Waziri wa Tamisemi, Ummy Mwalimu leo Septemba 10,2021, amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Mkoa wa Morogoro, Asajile Mwambambe ili kwenda kujibu tuhuma zinazomkabili katika Halmashauri ya Kilosa ya upotevu wa mabati 1,172.
Pia, Waziri Ummy amemuagiza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais — TAMISEMI kupeleka timu huru ya kuchunguza kwa kina suala la aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo.
Aidha Mhe. Ummy amewakumbusha watumishi wote wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kufanya kazi kwa weledi, kuwa waadilifu na makini katika utendaji kazi wao wa kila siku
June 29, 2021 Mwambambale alimuomba radhi mara tatu, aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Magufuli kwa kosa la kutotatua changamoto ya mgogoro wa ardhi wilayani humo.
Video: Mkurugenzi Kilosa Aomba Radhi Mara tatu Rais Magufuli
Mwambambale alilazimika kuomba msamaha huo, baada ya kuandamwa na malalamiko ya kutowajibika katika utatuzi wa migogoro, yaliyoibuliwa na wananchi wa wilaya hiyo katika ziara ya Rais Magufuli (enzi za uhai wake).
