×

Simba Yanga Azam Kuanzia Ugenini Ligi Kuu

RATIBA ya ligi kuu Tanzania bara imetangazwa leo Septemba 10,  na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) Almas Kasongo ambapo inatarajiwa kuanza kuanza kutimua vumbi rasmi Septemba 27,  huku vigogo Simba, Yanga na Azam Fc zitaanzia ugenini.

 

Mchezo wa kwanza kabisa utachezwa saa 8 mchana utawakutanisha Mtibwa Sugar na Mbeya Kwanza, Bingwa mtetezi Simba itakuwa ugenini kuvaana na Biashara United mechi itakayopigwa Mkoani Mara.

 

Timu ya Wananchi Yanga itakuwa Kaitaba kucheza na Kagera Sugar huku Azam Fc itakuwa ugenini kucheza na wagosi wa kaya Coastal Union.

 

Derby ya Kariakoo kati ya Yanga Dhidi ya Simba itakuwa Disemba 11, 2021.

Leave a Comment