×

Mahakama: Mali za Mmiliki wa Impala Hotel Zipigwe Mnada

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha, Masjala Ndogo ya Kazi imemuamuru Dalali wa Mahakama aliyepangwa kuhakikisha ifikapo Oktoba 15, mwaka huu awe ameuza mali za mdaiwa (mmiliki wa Hoteli ya Impala na Naura Springs) ili kufidia deni la Tsh bilioni 1.3 linalotokana na malimbikizo ya mishahara ya wafanyakazi.

 

Akitoa amri hiyo Naibu Msajili wa Mahakama hiyo Ruth Masama alidai kwamba makubaliano yaliyofikiwa na upande wa mdai na mdaiwa juu ya uuzwaji wa mali hizo ambazo ni kiwanja cha kitalu namba 16, 17, 18, 19, 20, 21, 22, na 23 vilivyopo eneo la Uzunguni Arusha na kwamba Oktoba 15 itapata taarifa ya utekelezaji wa zoezi hilo.

 

Afisa kazi Mfawidhi Mkoa wa Arusha, Emmanuel Mweta ameieleza Mahakama hiyo wamefika Mahakamani hapo kwa ajili ya kusajili mkataba wa maridhiano kwa ajili ya kuuza mali za mwajiri ili kufidia madai ya Wafanyakazi yanatotokana na malimbikizo ya Mishahara. Amesema viwanja hivyo vikiuzwa thamani yake inaweza kufikia zaidi ya Tsh billioni 2.

 

Mmiliki wa Hoteli za Ngurdoto, Impala na Naura Springs zote za jijini Arusha, Maleu Mrema alifariki dunia Julai 30, 2017 akiwa kwenye matibabu nchini Afrika Kusini.

 

Leave a Comment