
TIMU ya Manchester United imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 4-1 dhidi ya Newcastle United, game ambayo imemalizika hivi punde katika Uwanja wa Old Traford na kuwafanya mashabiki wa Man U kutoka vifua mbele huku wakitamba kuwa sasa ni zamu yao ya kunyakuwa Ubingwa wa Uingereza na makombe mengine.
Man U walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Critsiano Ronaldo kunako dakika ya nyongeza ya kipindi cha kwanza (45+2′) baada ya Mason Greenwood kuachia mkwaju uliomshinda kipa wa Newcastle, Freddie Woodman na kuutema kabla ya Ronaldo kuzamisha wavuni.

Hii iliamsha furaha kwa Man U kwani mashabiki walitamani Ronaldo afunge bao la kwanza katika mechi hii muhimu kwake ikiwa ni game ya kwanza kwake baada ya kurejea Man U akitokea Juventus, bao ambalo limedumu kwa kipindi cha kwanza cha mchezo huo.
Dakika ya Javier Manquillo, akaisawadhishia Newcastle baada ya kupokea pasi kutoka kwa Allan Saint-Maximin wakati wa moja ya counter attack waliyoifanya Nerwcastle.

Bao hilo la kusawadhisha liliongeza hasira kwa mashetani wenkundu ambapo dakika ya 62, Cristiano Ronaldo akaiandikia Man U bao la pili baada ya kupokea assist kutoka kwa Luke Shaw.
Haikutosha, dakika ya 80 Bruno Fernandes akafanya yake kwa kuiandikia Man U bao la tatu kufuatia assist ya Paul Pogba kabla ya Jesse Lingard kufunga ukurasa wa mabao wa Man U kunako dakika za nyongeza (90+2) akipokea asist ya Paul Pogba.
Man U sasa imekaa kileleni mwa Ligi Kuu ya Uingereza ikiwa na pointi 10 mbele ya Manchester yenye pointi 9, Brighton & Hove Albion ni ya tatu ikiwa na pointi 9 na Tottenham Hotspur ni ya nne, nayo ikiwa na pointi 9.