×

Mabaki ya Mwili wa Tupac Yalivutiwa Bangi

KWA kifupi tunaangalia mambo kumi ya kustaajabisha ya Tupac Shakur aliyefariki dunia Septemba 13, 1996 kwa kupigwa risasi huko Marekani.

 

Tupac alikuwa mwanamuziki mahiri wa Hip hop, rapa , mwigizaji, mtengeneza rekodi (record producer) mwanamashairi, mtunga filamu na mwanaharakati.

 

MOJA: Alipouawa, mwili wake uliteketezwa kwa moto (kwa mujibu wa tamaduni zao), cha ajabu wafuasi wake wa “outlaws” walichukua majivu yake, wakachanganya na bangi na kuvuta!

 

MBILI: Neno lake la mwisho kulisema kabla ya kifo chake ni neno “F*ck you!” alilomuambia askari aliyemuuliza ni nini kilikuwa kimemtokea.

 

TATU: Kinywaji alichokipenda zaid tupac kilikuwa Fanta orange. Alishawahi kuwafukuza badhi ya wafuasi wake nyumbani kwake kwa sababu eti walikuwa wanammalizia soda zake!

 

NNE: Akiwa mtoto mdogo akimkosea mama yake, alikuwa akipewa gazeti la New York Times alisome mbele ya mama yake!

 

TANO: Licha ya kuwa mwanafamilia nguli wa “West Coast”, cha kushangaza ni kwamba, Tupac alizaliwa New York ambako ni East Coast!

 

SITA: Alikuwa na uhusiano na msanii Madonna uhusiano ambao ulivunjika kutokana na Tupac kukashfiwa na watu weusi kwa kuwa na mpenzi mzungu!

 

SABA: Gazeti la Times, liliandika mahasimu wa Tupac,  B.I.G na P.diddy walijua kuwa Tupac angeuawa wiki moja kabla madai ambayo yalikanushwa na FBI.

 

NANE: Aliandika wimbo wa Dear Mama akiwa jela. Mama yake alishawahi kufungwa jela pia!

 

TISA: Kwenye wimbo wake wa “Me and My Girlfriend” anachozungumzia ni bunduki yake na si mpenzi wake kama inavyojulikana.

 

 

KUMI: Alijaribu maisha ya jela kabla hajazaliwa kwani mama yake alifungwa akiwa na ujauzito wa wake.

Stori na Richard Manyota

 

Leave a Comment