×

EX wa Rotimi Amuonya Vanessa

BAADA ya kutoa tangazo la ujauzito wake mapema wiki iliyopita, msanii maarufu wa Tanzania, Vanessa Mdee au Vee Money ameonywa kuwa asijipige kifua kuhusu mpenzi wake, Olurotimi Akinosho almaarufu Rotimi.

 

Mtangazaji Kim Oprah wa Nigeria ambaye aliwahi kuwa mchumba wa Rotimi (eksi) amemwambia Vanessa asione kama amepata kwani hana uhakika kwamba atabaki kuwa malkia wake milele.

 

Kupitia ukurasa wake wa TikTok, Oprah amemweleza Vanessa kuwa hata yeye kwa wakati mmoja alikuwa amekalia nafasi hiyo ambayo kwa sasa ameichukua na licha ya kuhakikishiwa kuwa yeye ni kila kitu kwake, lakini uhusiano wao haukudumu.

 

Oprah ametengeneza video ambayo inaonesha picha mbili tofauti, moja ikionesha Vanessa akiwa pamoja na Rotimi huku nyingine akimuonesha yeye akiwa pamoja na jamaa huyo enzi za uhai wa penzi lao.

 

Kwenye video hiyo, Oprah anaonekana akimnyooshea Vanessa kidole huku akisema; “Usiwe na starehe sana mpenzi, hata mimi nilikuwa kila kitu kwake!”

 

Hata hivyo, wanamitandao wengi hawajaridhishwa na kitendo cha Oprah huku wengi wakimwambia akubali hali ilivyo na asonge mbele na maisha yake. Jumatano iliyopita, Vanessa na Rotimi walitangaza kuwa wanatarajia mtoto wao wa kwanza wa kiume hivi karibuni.

STORI; MWANDISHI WETU

Leave a Comment