
Waziri Mkuu wa Haiti, Ariel Henry (kushoto) amemfukuza kazi Mwendesha Mashtaka aliyetaka kumfungulia mashtaka kama mshukiwa mmojawapo wa mauaji ya Rais Jovenel Moise (kulia) baada ya kugundulika kwamba Ariel aliongea kwa simu kwa dakika 7 na mpangaji mkuu wa mauaji ya rais huyo.
Imeelezwa kwamba, Claude alisema ushahidi unaonesha anamshuku Henry kwa kumpigia simu Badio, mawasiliano ambayo walifanya Julai 7, 2021 kati ya saa 4:20 asubuhi na ndiyo siku ambayo Rais Moise aliuawa nyumbani kwake na kundi la watu waliovamia makazi yake wakiwa wamejihami kwa silaha na kumshambulia yeye na mkewe kabla ya kumuaa.
Badio alikua jirani na nyumba ya Rais Moise wakati anapigiwa simu, Claude alisema. Aliongeza pia kwamba anahitaji kukutana na Henry kwa ajili ya mazungumzo ya kuwa kwa nini aliongea na Badio na baada ya hapo mauaji yakafuata.
Moise alimteuwa Henry kwenye nafasi ya uwaziri mkuu siku mbili kabla ya hajauawa. Henry hajazungumzia hali hiyo hadharani, lakini amewaeleza wanasiasa na viongozi wa Serikali kuwa anataka kujikita zaidi katika kutafuta wauaji halisi wa Rais Moise.
“Kuwa na uhakika, hakuna uharibifu, hakuna wito au mwaliko, hakuna ujanja, hakuna vitisho, hakuna kupambana na walinzi waliokuwepo, itanivuruga kutoka katika mipango yangu” amezungumza Henry kutokana na Shirika la Habari la AP.
Zaidi ya watu 40 wamemekamatwa mpaka sasa kwa kuhusishwa na mauaji ya Rais Moise wakiwemo raia wa haiti na Wanajeshi wa Colombia ambapo bado wanaendelea kumtafuta Badio (mshukiwa mkuu) na watuhumiwa wengine.