×

Ruto Akubali Kupatanishwa na Rais Kenyatta

MAKAMU wa Rais wa Kenya William Ruto ameafiki nia ya Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Kenya ya kumpatanisha na Rais Uhuru Kenyatta, limepoti gazeti la Daily Nation nchini humo.

 

Katika mazungumzo na viongozi wa kidini wa mashinani nyumbani kwake eneo la Karen Nairobi, Bw Ruto alisema yuko tayari na ana utashi wa kukutana na Rais Kenyatta.

 

Bwana Ruto alisema uhasama baina yake na rais ulisababishwa na “watu kutoka nje” ambao “walitaka kunufaika na serikali ambayo hawakuiunda .”

 

“Huwezi kudoea serikali ambayo hukuunda,” aliongeza Bw Ruto na kusema kuwa makubaliano ya Machi 2018 yanayofahamika kama ‘’handshake’’baina ya kiongozi wa chama cha upinzani cha ODM Raila Odinga na Rais Kenyatta yalikuwa chanzo.

 

Leave a Comment