
KUNDI la waasi wa Burundi wanaofahamika kama RED-Tabara wamesema eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bujumbura umeshambuliwa kwa muda wa takribani saa moja, siku ya usiku wa kuamkia Jumapili.
“Siwezi kuwaona, wako wapi?” – Kanali Floribert Biyereke, Msemaji Mkuu wa Jeshi la Burundi aliwaambia idhaa ya maziwa makuu ya BBC katika taarifa zake hivi karibuni.
Uwanja huu wa ndege uliopo mji mkuu wa kiuchumi ndio uwanja ambao ndege za kimataifa zinatua na kuondoka Burundi.

Taarifa ya shambulio kutokea Jumapili wakati Rais Evariste Ndayishimiye akiwa amepanga kuondoka kwenda New York katika mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa , akiwa rais wa kwanza wa Burundi kuhudhuria tangu mwaka 2011.
Kundi la waasi la RED-Tabara linadaiwa kufanya operesheni zake mashariki mwa DR Congo na kuhusiana na nchi jirani ya Rwanda, jambo ambalo serikali ya Rwanda ilikanusha.
Waasi hao walianza tangu kushindwa kwa mapinduzi ya mwaka 2015, wanasema wanapigania kuanzisha sheria ya utawala, na wamefanya mashambulio mabaya tofauti katika eneo la Burundi.