
MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Prince Dube, ameahidi kurejea kwa nguvu zote uwanjani baada ya kupona majeraha yake ya enka.
Akizungumza na Spoti Xtra, Dube alisema: “Baada ya kufanyiwa upasuaji, kwa sasa naendelea vizuri kuuguza jeraha langu, daktari ameniambia nitarudi baada ya wiki sita ila ikiwezekana naweza kurejea uwanjani mapema. Nitarudi na moto uleule.
“Washambuliaji waliopo ni wazuri sana na wanaisaidia timu kama unavyoona, nikipona nitapambana kuhakikisha narejea kikosini.”
ISAYA DANIEL