×

Roy Keane Aichambua Chelsea Vs Tottenham

MKONGWE wa Manchester United, Roy Kean amefungu­ka kuwa mch­ezo kati ya Tottenham na Chelsea ulikuwa kama wa wa­naume na wavu­lana.

 

Hii ni kuto­kana na na jinsi mchezo huo ulivy­okuwa kwa timu hizo za London na Chelsea ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0.

 

Chelsea walitawala katika mchezo huo kila idara ya kuifanya Tottenham kushindwa kutamba katika mchezo huo na wakipoteza kwa mara ya  pili mfululizo ndani ya ligi hiyo.

 

Mkongwe huyo alisema: “Chelsea walikuwa wanacheza katika ubora wa hali ya juu nadhani kwa walioangalia mechi watanielewa vizuri. Mchezo huu ulikuwa ni kama Wanaume vs Wavulana kutokana na Tottenham walivyocheza vibaya, sikuamini.

 

“Mambo kwa Tottenham hayakuwa vizuri japo kwenye soka mambo yanakuwa hivyo wakati mwingine kwani unaweza kupoteza na kukata tamaa kabisa.

 

“Kwa jinsi Tottenham walivyocheza kiukweli wamechukiza hawakuwa katika ubora kabisa makosa ambayo walifanya yaliwagharimu kwa kiasi kikubwa.

 

“Tottenham kwa sasa wameendelea kujiweka kwenye presha kubwa zaidi ndani ya kikosi hicho kutokana na mambo yanavyokwenda kikubwa wajipange nia kuangalia wapi kuna shida.”

LONDON, ENGLAND

Leave a Comment