TAHARUKI ya aina yake imetokea maeneo ya Scania, Kata ya Kiwalani jijini Dar baada ya watu wasiojulikana kuvamia na kuvunja vibanda vya machinga usiku wa kuamkia jana Septemba 23, 2021.
Global TV imefika eneo la tukio na kushuhudia jinsi vibanda hivyo vikiwa vimevunjwavunjwa huku bidhaa mbambali za wajasiriamali hao zikidaiwa kuchukuliwa na watu hao waliovunja kwa kutumia greda.
Tukio hili limekuja ikiwa ni siku chache baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla kutangaza kuwa machinga wote wanatakiwa kuondoka katika maeneo ya barabara kwani wasababisha adha kwa watumiaji wa barabara.
Kwa upande mwingine, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu alitoa agizo kwa machinga wanaopanga bidhaa zao kwenye milango ya maduka ya wafanyabiashara waondoke kwani wanawazuia wafanyabiashara hao kufanya biashara zao huku akiutaka uongozi wa jiji kuwaondoa kistaarabu na kuwapa maeneo mengine ya kufanyia biashara zao.