
WIKIENDI iliyopita kulipaswa kuwa na matukio mawili makubwa; moja Harmonize au Konde Boy Mjeshi alitangaza kumtambulisha msanii wake, Cheed ambaye tangu ajiunge na lebo yake ya Konde Gang alikuwa hajatambulishwa rasmi.
Tukio la pili ni la Rayvanny kumtambulisha msanii wake mpya aitwaye MacVoice, lakini Konde Boy Mjeshi aliahirisha tukio hilo huku Rayvanny akisisitiza shughuli ipo palepale na ikafanyika kibabe usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita.
Kitendo hicho cha Harmonize kimeibua gumzo kubwa baina ya timu za wasanii hao ambapo kimetafsiriwa na mahasimu wake kuwa huwenda alimkimbia Rayvanny kwa kuona kuwa atafunikwa.
Hata hivyo, habari za ndani zinaeleza kwamba, Konde Boy Mjeshi amesogeza tu siku hiyo ya kumtambulisha Cheed hadi atakaporejea kutoka kwenye ziara ya Marekani ili shughuli ya utambulisho iwe pambe.