
WASTARA Juma ni mwanamama anayetia huruma mno na huwa hakosi mambo ya kuhuzunisha kwa mashabiki wake kila uchwao.
Ukiacha mandhila mbalimbali aliyopitia huko nyuma ya kupata ajali na kukatwa mguu, kufiwa na mumewe Sajuki na kuolewa na kuachika mara kwa mara, mwenyewe anahisi si bure, kuna kitu, ama kuna jini au anafanyiwa mambo ya kichawi.
Kubwa kuliko ni kitendo cha kutoongezeka kwa mfuasi hata mmoja kwenye ukurasa wake wa Instagram kwa muda wa miaka minne, jambo ambalo Wastara anahisi ni mulemule kwenye mambo ya giza.