×

Bao la Mayele Lapikwa na Mataifa Matatu

MATAIFA matatu yalihusika kulipika bao pekee la ushindi lililofungwa na nyota wa Yanga, Fiston Mayele ambaye alizima furaha ya Simba kutetea taji la Ngao ya Jamii msimu huu.

 

Ilikuwa Septemba 25, Uwanja wa Mkapa ambapo kazi ilianza kwenye miguu ya taifa la Mali kupitia kwa kipa Diarra Djigui aliyepiga pasi ndefu iliyokutana na Mtanzania, Farid Mussa.

 

Utundu wa Mussa katika kuwakwepa mabeki wa Simba wakiongozwa na Pascal Wawa ulimfanya asisti yake ikutane na Mayele raia wa DR Congo ambaye alimtungua Aishi Manula.

LUNYAMADZO MLYUKA, DAR

Leave a Comment